21/05/2021
....TAMAA NI MBAYA! Yakobo 4:1-3....
Ni kitu gani kinachosababisha vita na ugomvi miongoni mwenu? Je, si tamaa zenu zinazopingana ndani yenu? Mnatamani lakini hampati kwa hiyo mnaua . Na mnatamani kupata lakini hampati vile mnavyotaka kwa hiyo mnapigana na kuanzisha vita. Mmepungukiwa kwa sababu hamumwombi Mungu. Mnaomba lakini hampokei kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mtumie mtakavyopata kwa kutosheleza tamaa zenu. Tamaa ni mbaya, imefanya wengine wauwe, imesababisha watu kuwa na ugomvi na vita na hii tamaa ndio inasababisha tukiomba tusipewe. Mungu hawezi kukupa unachoomba ikiwa una nia mbaya ama ukipewa unaenda kuanzisha vita, hutapewa. Acha tamaa, omba Mungu kwa roho Safi, ukipewa usianzishe vita wala ugomvi na utazidi kupewa. Uwe na wikendi ya baraka majaliwa tuonane Jumapili tupeperushe bendera ya 5am for 10am. Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili