02/07/2017
MTAJI..Neno mtaji ni neno linalojirudia rudia katika kila hotuba, mjadala au mahojiano ya vijana mbalimbali nchini na Duniani kwa ujumla, inaaminika kuwa Mtaji ndio kikwazo cha vijana wengi kushindwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kijasiliamali, ni kweli ni moja ya changamoto inayopelekea vijana wengi kubweteka hali inayo pelekea vijana kuishi maisha yasiyotamanika katika jamii, lakini naomba ifahamike kuwa mtaji ni mtaji nikiwa na maana kuwa wazo ulilonalo laweza kuwa mtaji, mda ulionao waweza kuwa mtaji, akili yako ni mtaji, pia watu na vitu vinavyo kuzunguka vyaweza kuwa mtaji vikitumiwa kwa ufasaha na ufanisi wake japo vyaweza kuto kuwa katika hali ya kifedha (cash money) ila vikitumika kimanufaa vya weza kuzaa fedha na mwishowe kubadili historia ya maisha yako na ukawa mtu mwingine kabisa katika tasnia hii ya ujasiliamali..pia nataka kushare nanyi kuwa kiasi chochote cha fedha chaweza kuwa mtaji si lazima uwe na kiwango kikubwa cha fedha ndio ufungue biashara au mradi k**a wanavyo fikiri vijana wengi..waweza anza na kilicko mkononi na kisha kikakupeleka katika hatua nyingine ambayo hukuwahi kuifikiria hata wakati wa zama za musa Mungu alimuuliza musa "una nini mkononi" musa akajibu nina fimbo" Mungu akasema piga mwamba mara tatu kisha wakapata maji...hii ni kudhihirisha kuwa cha kuthamini ni kile ulichonacho mkononi kwa sasa na si kile unacho kifikiria kwani ili ukifikie lazima uanze hatua na hiki kidogo ulichonacho...